NINI TUNAFANYA

Takriban  miongo 3  ya utafiti katika magharibi ya bahari ya hindi imetupelekea kuamini kwamba kuna nguva wachache sana waliobakia. Mradi huu wa WIOMSA uliandaliwa kubaini kama nguwa bado wapo katika bahari ya afrika mashariki na kama wapo, wapo wangapi na njia bora ya kuwahifadhi wasije wakatoweka.

Tunategemea kukamilisha hili kwa awamu

Kwanza, kwa kutumia ripoti na taarifa  za kihistoria, tumebaini maeneo ambapo nguva wapo. Kwa kutumia taswira ya satalaiti na ripoti juu ya  wingi na aina ya nyasi bahari, tumebainisha sehemu gani  nguva wanaweza kuwepo au wapo. Kwa kutokana na taarifa hizi ambazo tumezipata tumekuja na MAENEO MUHIMU (maeneo ambayo tunahisi nguva bado wapo)

Pili, tunahitaji kubaini kama nguva bado wapo katika hayo MAENEO MUHIMU (HOT SPOTS) na kama wapo je nikawaida yao kuwepo (wingi), au sio kawaida yao kuwepo. Kufanikisha hili tunaongea na jamii, wavuvi, wazee na wanawake (wanaotayarisha chakula). Tunawauliza kama wanawaona nguva? Sehemu gani  wanawaona na mara ngapi wanawaona. Huwa tunatumia dodoso kukusanya taarifa za aina hii.

Kiukweli kma jamii haioni nguva haimaanishi kwamba hawapo lakini mara nyingi inakuwa kweli. Tunachokifanya huwa tunaweka kinasa sauti chini ya maji ambacho hunasa sauti za nguva  kama wapo. Kutokana na maelezo ambayo jamii imetupatia na kwa kuangalia mara ngapi tuinasikia sauti za nguva, tunapata uwelewa kama wapo au hawapo.

Katika maeneo ambapo nguva imesemekana wapo, huwa tunatumia ndege kuwahesabu wapo wangapi. Hii kwa kweli haiwezekani sana lakii inapowezekana tunafanya hivyo

Mwishowe kutokana na matokeo ya utafiti wetu, tunahitaji kupata njia za kujaribu kuwahifadhi nguva tunaowaona. Ili kufanikisha hili tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja  jamiii na taasisi husika na hapo ndipo penye changamoto. Kutoa mapendekezo kwa taasisi au mamlaka husika ni rahisi, lakini kuyatekeleza si jambo rahisi. Pia ni ngumu zaidi kwa jamii ambayo inategemea maeneo ya mwambao kwa ajili ya maisha yao, kubadilisha tabia zao  ili nguwa waweze kuhifadhika pamoja na maeneo wanayoishi. Hii awamu ya mwisho ni ngumu lakini tunatumainia kukubiliana nayo pindi tu tutakapopata taarifa zenye kuaminika.